ZINAZOVUMA:

Odinga amuonya balozi wa Marekani

Raila Odinga amemuambia balozi wa Marekani kuwa Kenya sio koloni...

Share na:

Kiongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja nchini Kenya Raila Odinga, amemjibu Balozi wa Marekani Mchini humo Meghan Whitman, kuwa Kenya sio koloni la Marekani na kumtaka Whitman kujiepusha na siasa za Kenya, la si hivyo watafanya mazungumzo ili arudishwe nchini kwake.

Hili limetokea baada ya Balozi Whitman kusema kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 ulikuwa huru na wa haki, na Rais William Ruto alimshinda Odinga kwa njia ya haki.

Akizungumza katika Mkutano huko Eldoret Odinga amesema, “Nataka kumwambia balozi huyu acha Wakenya waendelee na mambo yao”.

“Ikiwa Maandamano yanaweza kuleta mazungumzo kati ya Serikali na Upinzani basi kila kitu kiko sawa na Maandamano”.

Aidha Odinga alisisitiza kuwa, “Mwambieni balozi huyu Kenya sio Marekani, Kenya sio koloni la Marekani, funga mdomo wako au tutakurudisha nchini kwako”

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya