ZINAZOVUMA:

Niger waandama kuunga mkono uongozi wa kijeshi

Wananchi nchini Niger wameandamana wakiishtumu Ufaransa na kulaani vikwazo vilivyowekwa...

Share na:

Maelfu ya raia wa Niger, wameandamana jana jijini Niamey, kuunga mkono uongozi wa kijeshi uliomwondoa madarakani, Rais Mohammed Bazoum mwezi uliopita.

Waaandamanaji hao wakiwa wanapeperusha bendera ya nchi yao, ile ya Urusi, China na India, walisikika wakiishtumu nchi ya Ufaransa kwa kutaka kuvunja Amani na kulaani vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS.

Aidha, waandamanaji hao walisikika wakisema hawaungi mkono mpango wa nchi za ECOWAS kuivamia nchi yao, ili kumrejesha madarakani Rais Bazoum.

Maandamano hayo yamefanyika siku moja tu baada ya ujumbe wa ECOWAS ukiongozwa na aliyekuwa kiongozi wa kijeshi nchini Nigeria, Abdulsalami Abubakar kuzuru jijini Niamey kwa ajili ya mazungumzo.

Ujumbe huo ulikutana na uongozi kijeshi na Rais Bazoum, huku kiongozi wa ujumbe huo akisema baada ya mazungumzo hayo bado kuna tumaini la kupata mwafaka kwa njia ya mazungumzo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya