ZINAZOVUMA:

Niger inatarajiwa kufikia makubaliano na ECOWAS

Waziri Mkuu alieteuliwa nchini Niger amesema kuwa mazungumzo baina yao...

Share na:

Waziri Mkuu mpya wa Niger amesema kuna matumaini ya kufikia makubaliano baina ya uongozi wa jeshi nchini humo na Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Magharib ECOWAS.

Ali Mahamane Lamine Zeine, aliyeteuliwa kwa hivi karibuni na serikali ya kijeshi, alikuwa akizungumza kwa mara ya kwanza hadharani katika mkutano na wandishi habari katika mji mkuu Niamey.

“Hatujasitisha mazungumzo na ECOWAS, bado tunaendelea kujadiliana. Tuna matumiani ya kufikia makubaliano katika siku zijazo,” aliwaambia wandishi habari.

Jumuiya ya Ecowas imetishia kutumia nguvu kurejesha utawala wa kiraia nchini humo baada ya jeshi kufanya mapinduzi mnamo Julai 26 na kumng’oa madarakani Rais Mohamed Bazoum.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya