Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imetangaza nafasi za ajira 524 ili kujaza nafasi mbalimbali ikiwa ni pamoja na nafasi 206 za maofisa wasimamizi wa kodi.
Tangazo la TRA lililochapishwa na gazeti la Daily News limeorodhesha idadi ya nafasi hizo na vigezo kwa waombaji na kwa ujumla waombaji wanapashwa kuwa tayari kufanya kazi popote pale katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Waombaji wote lazima wawe raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale ambao ni katika Utumishi wa Umma,” taarifa ya Kamishna Jenerali Mamlaka ya Mapato Tanzania imesema.
Mwisho wa kutuma maombi ni Juni 9, 2023