Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) iliyopo chini ya wizara ya kilimo imewakamata wafanyabiashara wanne wa sukari kwa kuuza bidhaa hiyo bila kufuata bei elekezi kwa kanda ya ziwa bei ya rejareja ni shilingi 2800 hadi elfu 3000.
Maafisa wa bodi hiyo wakiongozwa George Gowelle wamefanya msako katika jiji la Mwanza na kuwakamata wafanyabiashara hao na kubaini kuwa wanauza sukari kwa bei ya zaidi ya shilingi elfu 4000 kinyume na taratibu.
Akizungumza mara baada ya msako huo, Afisa wa bodi ya sukari Tanzania, George Gowelle amesema wafanyabiashara wanapaswa kuuza sukari kwa bei elekezi iliyowekwa na bodi.