ZINAZOVUMA:

Museven asema sheria haitobadilika

Raisi wa Uganda amesema sheria aliyoitia saini imekamilika na hakuna...

Share na:

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameelezea kuhusu upinzani wanaoupata kutoka jumuiya ya kimataifa dhidi ya sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja aliyotia saini.

Raisi Museveni amesisitiza kuwa kutiwa saini kwa sheria hiyo ni makubaliano yaliyokamilika na haitawezekana kubadilishwa.

“Utiaji saini wa Muswada wa Kupinga mapenzi ya jinsia moja umekamilika, hakuna mtu atabadilisha hatua yetu. Tunapaswa kuwa tayari kwa vita,”

Raisi Museveni aliyasema hayo katika taarifa yake baada ya mkutano na wanachama wa chama chake cha National Resistance Movement (NRM).

“NRM haijawahi kuwa na lugha mbili, tunachokuambia mchana ndicho tutakuambia usiku,” aliongeza.

Hii inakuja huku kukiwa na shutuma kutoka kwa mataifa ya Magharibi na makundi ya haki za binadamu dhidi ya hatua aliyoichukua Raisi Museveni.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya