ZINAZOVUMA:

Mtoto wa miaka 12 akamatwa kwa ulawiti Njombe

Mtoto wa miaka 12 ashikiliwa na Polisi mkoani Njombe kwa...

Share na:

Jeshi la polisi mkoa wa Njombe linamshkilia mtoto mwenye umri wa miaka 12, kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi mwenye umri wa miaka 10 katika shule iliyopo Makambako mkoani Njombe.

Hayo yameelezwa leo April 13, 2024 na Kamanda wa Polisi mkoa Njombe, Mahamoud Banga wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema tukio hilo limetokea April 4, 2024 katika mtaa wa jeshini mjini Makambako, ambapo mwanafunzi huyo alikuwa akilawitiwa kwa ahadi ya kupewa fedha na mtuhumiwa huyo ambaye aliacha shule akiwa darasa la sita.

Aidha Kamanda Banga amesema, mwanafunzi huyo alikuwa akifanyiwa vitendo hivyo kwa muda mrefu, lakini hakusema kwa wazazi wake mpaka wazazi walipogundua kuwa anatokwa na hajakubwa na mama yake kumuadhibu ndipo aliposema kuwa anafanyiwa vitendo hivyo.

Chanzo: Mwananchi

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya