ZINAZOVUMA:

Msafara wa amani washambuliwa Somalia.

Msafara wa wasuluhishi amani wa umoja wa Afrika umeshambuliwa katika...

Share na:

Msafara wa wasuluhishi wa amani wa umoja wa Afrika umeshambuliwa kwa bomu siku ya jumatatu katika mji mkuu wa Mogadishu nchini Somalia.

Taarifa zinasema mpaka sasa watu watatu wanaripotiwa kupoteza maisha kutokana na mlipuko huo.

Majeshi ya umoja wa Afrika yamekuwepo Somalia kulinda amani wakati shambulio hilo likitokea ambapo taarifa za ulinzi zinasema bomu hilo lilitegwa jirani na njia iliyokua ukipita msafara huo.

Hakuna kundi lolote ambalo limetajwa kuhusika na shambulio hilo mpka sasa hata hivyo kundi la Al Shabaab limekua likihusika na mashambulizi ya hivi karibuni.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya