ZINAZOVUMA:

Monduli: Mbunge aahidi vitanda sekondari ya Oltinga

Mbunge wa Monduli Fredirick Lowassa aahidi kutoa vitanda vya bweni...

Share na:

Mbunge wa jimbo la Monduli Fredrick Lowassa ameahidi kuchangia vitanda katika shule ya sekondari Oltinga.

Ahadi hiyo aliitoa katika ziara yake kwenye kata ya Selela iliyopo jimboni kwake.

Lengo la ziara hiyo ni kukagua miradi ya maendeleo, utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na kusikiliza na kutatua Kero Mbalimbali za Wananchi.

Alitoa ahadi hiyo katika ukaguzi wa jengo jipya la Bweni katika Shule ya Sekondari Oltinga,  baada ya kusomewa taarifa ya jengo hilo kuwa kuna uhitaji wa vitanda 104.

Mbunge huyo alikubali kuichukua changamoto hiyo na kuifanyia kazi kwa kutoa vitanda hivyo ili wanafunzi wapate pa kulala.

“Tumefika hapa tumetembea na tumezungumza na wanafunzi, Risala ikasomwa lakini la msisitizo zaidi ni changamoto ya bweni letu ambalo halina vitanda, kitu ambacho tunapaswa wote kujua Shule ya Oltinga ilianzishwa mwaka 2007, Shule ya Oltinga ni mmoja kati ya waasisi wa Shule za kata nchi nzima. Wakati mzee Lowassa anataka kuanzisha shule za kata nchi nzima alisema lazima kwanza aaanze na jimbo lake, kwa hiyo nilipofika pale nikasema pamoja na Changamoto nyingine na mimi nataka niache alama katika Shule hii ya Oltinga kwa kutoa vile vitanda 104 kulingana uhitaji wa Mwalimu Mkuu katika taarifa yake” Amesema Fredrick Lowassa

  “Tumetoka hapo tukaenda kwenye tank kubwa hili hapa ambalo linatoa maji lositeti, nimeambiwa tank hili lilijengwa Mwaka 1951 na Wajerumani ili kusaidia mifugo kupata  maji wakati ule.

Mwaka 51 hata mzee Lowassa alikuwa hajazaliwa, lakini lazima tukubali teknologia ya wenzetu pamoja na changamoto ndogondogo za tank lile bado linaonekana lina uimamara sana.

Nguvu za wananchi ni kubwa kujenga eneo la mifugo kunywea Maji na Ripoti nimeona hongereni sana na kwa changamoto zilizobakia nimechukua ili kuzifanyia kazi” Amesema Fredrick.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya