ZINAZOVUMA:

Mwili wa Edward Lowassa kuagwa

Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Lowassa anatarajiwa kuagwa katika viwanja...

Share na:

Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Lowassa anatarajiwa kuagwa katika viwanja viwili vikubwa kikiwemo cha Sheikh Amri Abeid jijini Arusha na baadae kupumzishwa kijijini Kwake wilayani Monduli.

Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ratiba ya mazishi ya Edward Lowassa.

Vilevile, Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiye anayetarajiwa kuongoza Mazishi ya Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Lowassa yanayotarajiwa kufanyika Wilayani Monduli Mkoani Arusha Jumamosi Februari17, 2024.

Awali Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alitangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa ambapo bendera zitapeperushwa nusu mlingoti kuanzia tarehe 10 Februari, 2024.

Amesema katika kipindi cha siku tano za maombolezo, Taifa litaendelea na shughuli za umma na kijamii sambamba na kushirikiana na wanafamilia katika ratiba ya msiba kama ilivyoandaliwa na kamati ya mazishi ya Kitaifa na wanafamilia.

Amesema ratiba inaonyesha Jumanne Februari 13, 2024 mwili wa Hayati Lowassa unatarajiwa kuangwa na viongozi na wananchi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema Jumatano Februari 14 mwili wa Hayari Lowassa utapelekwa katika Kanisa la KKKT Azania Front kwa ajili ya ibada takatifu na kuaga.

Amesema Alhamisi Februari 15 mwili wa Hayati Lowassa utasafirishwa hadi jijini Arusha ambapo viongozi na wananchi watapa fursa ya kuaga katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid.

Waziri Mkuu huyo mstaafu alifariki jana (Jumamosi, Februari 10, 2024) wakati akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam na tangazo la kifo chake lilitolewa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya