ZINAZOVUMA:

Mkongwe wa vichekesho Nollywood afariki na miaka 62

Wiki chache baada ya kufariki Mr. Ibu, msanii mwingine wa...

Share na:

Nguli wa vichekesho vya Nollywood Amaechi Muonagor amefariki akiwa na umri wa miaka 62.

Alifariki siku ya Jumapili baada ya kushindwa kwa figo na alikuwa kwenye matibabu ya dialysis, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Kifo chake kimekuja siku chache tu baada ya kuomba msaada wa kutafuta fedha kwa ajili ya kupandikiza figo nchini India .

Mashabiki wake wengi wamejitokeza kwenye mitandao ya kijamii kumuomboleza.

Wakati wa kazi yake, Muonagor alionekana katika filamu nyingi, ikiwa ni pamoja na Aki na Paw Paw, mojawapo ya majukumu yake maarufu ambapo aliigiza kama baba wa vijana wawili watundu , waliojawa na furaha kupita kiasi.

Aliteuliwa kuwania Tuzo za Africa Magic Viewers’ Choice 2017 kwa Muigizaji Bora.

Kifo chake kimakuja wiki chache tu baada ya Nigeria kumpoteza nyota mwingine wa Nollywood John Okafor, anayejulikana zaidi kama Mr. Ibu, ambaye pia alihitaji msaada wa matibabu .

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,