ZINAZOVUMA:

Mjukuu wa Nelson Mandela afariki kwa saratani

Mjukuu wa Rais wa kwanza wa Afrika Kusini Nelson Mandela...

Share na:

Mjukuu wa Baba wa Taifa la Afrika Kusini Nelson Mandela anaeitwa Zoleka Mandela amefariki dunia kwa saratani akiwa na umri wa miaka 43.

Familia ya Mandela imetangaza taarifa hiyo kwenye mtandao wa ‘Instagram’ wa msemaji wa familia na kueleza kuwa Zoleka alifariki jana Jumatatu Septemba 25, 2023 jioni, akiwa amezungukwa na ndugu, jamaa na marafiki.

Katika miaka ya hivi karibuni Zoleka alijulikana sana kwa kuelezea matibabu yake ya saratani na pia kuwa wazi juu ya historia yake ya uraibu wa dawa za kulevya na mfadhaiko zilivyomletea madhara zaidi.

Si hivyo tu, lakini pia aliwekwa wazi kuhusiana na changamoto aliyoipata ya kunyanyaswa kingono wakati akiwa mdogo.

Zoleka aligundulika kuwa na saratani ya matiti, takribani miaka kumi iliyopita, na alikuwa akipata matibabu na hali yake ilizidi kuimarika, japo baadaye hali ilibadilika.

Mwaka jana, alithibitisha kuwa alikuwa na saratani kwenye ini na mapafu, kisha ikasambaa kwa viungo vingine, na alikuwa akipata matibabu na alilazwa Septemba 18, 2023.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya