ZINAZOVUMA:

Milioni 5 tu mnyama kuitwa kwa jina lako

Shirika la Hifadhi za Taifa za Tanzania Tanapa limeanzisha utaratibu...

Share na:

Baada ya wanyama kupewa majina ya watu maarufu wa nje ya nchi, Shirika la Hifadhi za Taifa za Tanzania (Tanapa) limeanzisha utaratibu maalumu wa kuwezesha watu wanaotaka baadhi ya wanyama waitwe majina yao kufanya hivyo lakini kwa kulipia Sh5 milioni.

Utaratibu huo nakuja baada ya baadhi ya wanyama akiwemo simba aliyepewa jina Bob Juniour, faru aliyepewa Faru John na Rajabu.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Julai 24, 2023 na Kamishina wa Uhifadhi wa Tanapa, William Mwakilema wakati akielezea utekelezaji wa majukumu na mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu kwa mwaka 2023/24.

“Tumeanzisha utaratibu wa kuwapa majina baadhi ya wanyama lakini sio bure. Na hawa wanyama sio wote labda kama umesema kuwa unampenda sana fisi unataka huyo fisi awe na jina lako,”amesema.

Amesema bodi ya menejimenti ya Tanapa imeshapitisha utaratibu huo ambao utaanza na wanyama aina ya faru.

Pia amesema mtu yoyote ambaye anataka aendelee kumuona anaweza kumuasili na atatakiwa kuchangia gharama za kumuhifadhi za Sh1 milioni kila mwaka.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya