ZINAZOVUMA:

Mgombea urais Marekani aahidi kusitisha msaada Ukraine

Mgombea wa nafasi ya urais nchini Marekani kupitia chama cha...

Share na:

Wakati vuguvugu la Uchaguzi Mkuu wa Marekani wa mwaka 2024 likianza kushika kasi, watia nia nane wa kiti cha Urais kwa chama cha Republican, usiku wa kuamkia leo Alhamisi Agosti 24, 2023, wamechuana vikali katika mdahalo wa kunadi sera zao huku kivutio kikubwa kikiwa kwa mwanasiasa Vivek Ramaswamy na sera zake za kutounga mkono msaada wa nchi hiyo kwa Ukraine.

Ramaswamy amesema endapo atachaguliwa kuwa Rais, hataunga mkono msaada wa ziada kwa Ukraine hasa katika vita yao dhidi ya Russia huku akiitaja hatua hiyo kama kupoteza rasilimali za nchi hiyo.

“Msaada wa Marekani kwa Ukraine ni hasara kubwa na rasilimali zinazoenda Kyiv zinapaswa kutumika ndani ya nchi,” amesema katika mjadala huo.

“Hili ni janga, tunalinda dhidi ya uvamizi kwenye mpaka wa mtu mwingine, wakati tunapaswa kutumia rasilimali hizo hizo za kijeshi kuzuia uvamizi katika mpaka wetu wa kusini hapa kwetu,” ameongeza.

Hata hivyo, kauli hiyo ilipingwa vikali na Mwanadiplomasia na mwanachama wa chama hicho Nikki Haley aliyemuita Ramaswamy kuwa mtu asiye na uzoefu katika diplomasia.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,