ZINAZOVUMA:

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha Mawaziri

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la...

Share na:

Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud wa Saudi Arabia ameongoza mkutano wa baraza la mawaziri siku ya Jumanne, baada ya kupatiwa matibabu ya mapafu kwa muda tangu wiki iliyopita.

Taarifa hiyo ya Mfalme Salman kuongoza kikao hicho, ilitolewa na shirika la Habari la Saudi.

Pia kwenye kikao hicho kilichofanyika kwa Video, Mrithi wa kiti cha ufalme Mohammed bin Salman alikuwa pamoja na baba yake.

Mwanzoni mwa mkutano huo, Mfalme Salman aliwashukuru watu wa Saudi kwa salamu zao za heri na maombi yao ya upole.

“Pia alitoa shukrani zake kwa kila mtu aliyemtumia salamu za kumuombea afya njema na ustawi kutoka kwa viongozi wa nchi ndugu na rafiki, akiomba Mwenyezi Mungu awape kila mtu afya njema na furaha,” ilisema taarifa ya baraza hilo kupitia Saudi Press Agency.

Jumba la kifalme lilisema kuwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 88, atatibiwa na antibiotiki hadi ugonjwa utakapopungua, kulingana na vipimo vya Kasri la kimatibabu la Al Salam.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya