ZINAZOVUMA:

Messi atambulishwa rasmi Miami

Lionel Messi rasmi sasa atambulishwa katika klabu yake mpya ya...

Share na:

Nyota wa Argentina na mshindi wa kombe la dunia mwaka 2022 Lionel Messi ametambulishwa rasmi kwa mashabiki wa klabu yake mpya ya Inter Miami katika uwanja wa DRV PNK usiku wa Jana.

Umati wa mashabiki zaidi ya 20,000 uliokua umenunua tiketi uliweza kumuona mshindi huyo mara saba wa Ballon d’Or akipewa jezi namba 10.

Katika hotuba fupi ya aliyoitoa kwa lugha ya Kihispania, Messi, 36, aliwashukuru mashabiki hayo na kusema kuwa alikuwa na hamu sawa sana kukutana nao.

Lionel Messi anajiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Soka ya nchini Marekani kwa mkataba wa miaka miwili hadi mwisho wa 2025.

Messi ataungana tena na kiungo wa kati wa Barcelona Sergio Busquets – ambaye alicheza naye Barcelona ambaye pia amesajiliwa na klabu hiyo ya Miami hadi 2025.

Messi alitambulishwa kama ndio namba 10 Bora zaidi kuwahi kutokea Marekani na duniani.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya