ZINAZOVUMA:

Mechi ya Yanga yasogezwa mbele

Shirikisho la mpira nchini Tanzania TFF limeisogeza mbele mechi ya...

Share na:

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesogeza mbele mchezo namba 096 wa hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) kati ya Singida BS dhidi ya Young Africans uliopangwa kuchezwa Mei 7, 2023 katika uwanja wa Liti, Singida mpaka hapo utakapopangiwa tarehe nyingine.

Mabadiliko hayo yametokana na maombi ya klabu ya Young Africans kupitia barua Kumb. Na. YASC/TFF 2023/120 kuomba kupata muda zaidi wa maandalizi ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini utakaochezwa Mei 10, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

TFF kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi imekubali kusogeza mbele mchezo huo na utapangiwa tarehe nyingine.

Katika hatua nyingine, TFF imeusogeza mbele kwa siku moja mchezo namba 095 wa hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) kati ya Azam FC dhidi ya Simba SC uliopangwa kuchezwa Mei 06, 2023 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara kwenda Jumapili Mei 7, 2023.

Mabadiliko haya yamefanyika ili kutoa nafasi kwa timu za Azam FC na Simba kupata muda zaidi wa maandalizi kuelekea katika mchezo huo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya