ZINAZOVUMA:

MCHECHU: Makampuni 28 yatajitegemea

Mabadiliko makubwa ya kiutndaji yamefanyika katika kikao kazi baina ya...

Share na:

Bw. Nehemia mchechu Msajili wa Hazina ametoa taarifa kuwa, hadi mwishoni mwa wiki hii, inatarajiwa kampuni 28 za serikali kujiendesha bila utegemezi wa serikali.

Pamoja na kuwa haijatajwa orodha kamili ya kamuni hizo, imedokezwa kuwa Shirika la maendelea ya Petroli (TPDC) na Shirika la Madini (STAMICO) ni katika kampuni hizo 28.

Katika kuongezea Bw. Mchechu amesema kuwa, mabadiliko haya yanatokana na vuguvugu la mabadiliko katika taasisi za umma nchini.

Kutokana na maneno hayo inatazamiwa taasisi nyingine, kuongezwa katika orodha hiyo ya taasisi 28 zinazotarajiwa kuanza kujitegemea wiki hii.

Na tayari kuna taasisi nyingine zimeomba kuongezewa miaka miwili kabla ya kuanza kujitegemea.

Na Bw. Mchechu amesema kuwa, haya ni maamuzi waliyokubaliana na wenyeviti wa bodi pamoja na watendaji wakuu wa taasisi hizo.

Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Mpango na Uwekezaji, alielezea kuwa serikali imeanza kufanya mageuzi katika mashirika ya umma.

Mbali na hatua hii pia wameajiriwa wataalamu wenye ujuzi na utamaduni wa kampuni ili kuboresha jumla ya utendaji wa mashirika haya.

Wakati anapokea taarifa hiyo ya mabadiliko ya kiutendaji kutoka hazina, Raisi Samia amekemea mazoea ya Mawaziri na Makatibu wakuu, kuweka mashinikizo kwa taasisi za umma kutoa fedha nyingi kwa ajili ya shughuli za kiutawala.

Raisi Samia alisema kuwa mashinikizo hayo yakipungua au kuondoka ndio ufanisi utaongezeka katika taasisi hizo za umma.

Katika kuweka wazi mategemeo yake kwa hatua hii kwa washiriki, Rais Samia alisisitiza umuhimu wa jitihada za kujenga uzalishaji bora wa mashirika haya kwa kusema “Natarajia mtatenda kazi kwa bidii ili kufikia mafanikio katika mashirika haya. Nina matarajio makubwa kuhusu utendaji wenu.”

Aidha, alimwagiza Msajili wa Hazina Bw. Mchechu, kuweka mikataba inayobainisha matarajio ya utendaji kwa mashirika haya ya umma.

Kwa taasisi za umma zilizofanya vizuri kwa mwaka wa fedha 2022/2023, zitapewa tuzo ya utendaji bora na Raisi Samia kama taarifa ya hazina ilivyobainisha.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya