ZINAZOVUMA:

Marekani kushtakiwa na makampuni ya Ulaya

Kampuni ya marekani yafunguliwa mashtaka kwa kuvunja mkataba na kampuni...
Venture Global

Share na:

Kampuni ya Venture Global ya nchini Marekani imefunguliwa mashataka na kampuni kadhaa za ulaya.

Kampuni hizo zimefungua kesi hiyo kudai gesi, kutokana na Mkataba wa kuletewa gesi na kampuni hiyo.

Makampuni ya ulaya yaliyofungua kesi dhidi ya Venture Global, ni Shell na BP za Uingereza, Eni na Edison za Italia na Repsol ya Hispania.

Lengo la kampuni hizo kuingia kununua gesi toka marekani, ni kupunguza utegemezi wa gesi toka Urusi.

Hata hivyo baada ya makubaliano hayo, Venture Global ilivunja makubaliano yao na kuuza gesi kwa mnunuzi wa bei ya juu katika soko (spot Market).

Katika utetezi wake Venture global, imesema kuwa mitambo ya kuchakata gesi ya Calcasieu Pass LNG haizalishi kulingana na matarajio yao.

Na haikukataa kuwa imeuza shehena 200 za gesi ya kimiminika (LNG) katika soko, huku ikiwa haija kidhi mahitaji ya wateja wa mikataba kutoka ulaya.

Hali inayosababisha kukosa gesi ya LNG inayotosha wateja wake wa Ulaya walioingia nao mkataba.

Mitambo ya Calcasieu Pass ni uwekezaji uliofanywa na Venture Global, kugandamiza na kupoza gesi asilia hadi kufikia kuwa kimiminika.

Na mtambo huo una uwezo wa kuzalisha Tani Milioni 10 gesi ya kimiminika kwa mwaka.

Hadi sasa mamlaka za Marekani na Ulaya hazijasema jambo juu ya sakata hilo.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,