ZINAZOVUMA:

Mambo moto kesi ya bandari

Mawakili wa pande zote wakubaliana mambo sita muhimu ambayo mahakama...

Share na:

Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya leo Jumatano Julai 26, 2023 inaanza rasmi kusikiliza kesi ya makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai (IGA) yanayohusha uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam kupitia kampuni ya Dubai Ports World (DP World).

Jana Julai 25, 2023, mawakili wa pande zote na Mahakama walikubaliana mambo sita kama viini vikuu vya kesi hiyo ambavyo mahakama inapaswa kuvitolea uamuzi.

Leo Julai 26, 2023, upande wa madai unaanza kuchambua viini hivyo kuthibitisha madai yao ya ubovu wa masharti ya makubaliano hayo, wakati wadaiwa watakuwa na kibarua cha kupangua hoja hizo kuonyesha kwamba masharti ya makubaliano hayo yako sawa na yamezingatia maslahi ya Taifa.

Kumekuwa na hoja nyingi kwenye mitandao ya kijamii, majukwaa ya kisiasa, mtu mmoja mmoja, makundi na au taasisi zinazoskinzana katika makubaliano hayo, huku kila upande ukijitahidi kuushawishi umma kuamini mtazamo wake.

Hata hivyo, hoja zinazotolewa leo ndizo rasmi zitakazowekwa kwenye kumbukumbu ya kudumu na ndizo zitakazoamua hatima ya makubaliano hayo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya