Raisi Samia Suluhu Hassani amteua Gerson Msigwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Msigwa amechukua nafasi ya Said Othman, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
Kabla ya uteuzi huo Gerson Msigwa alikuwa ni Mkurugenzi wa idara ya Habari – Maelezo na pia Msemaji Mkuu wa Serikali.
Msigwa ameshika nyadhifa hizo kwa pamoja tangu Aprili 2021 ambapo kabla ya nafasi hizo, alikuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu.