Anaandika Dkt.Ahmad Sovu
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania-kazi iendelee
Jana tarehe 07/09/2023 timu ya Tanzania 🇹🇿 maarufu Taifa Stars 🌟 imefanikiwa kufuzu kushiriki kucheza fainali za kombe la Afrika.👏👏👏
Stars wamefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kutoka suluhu na timu ya Taifa ya Algeria.
Watabe wa mambo ya soka wanakwambia si jambo rahisi kushinda ugenini hasa katika nchi za Kaskazini mwa Afrika kama Algeria. Wenyewe huviita viwanja vigumu.
Heko Taifa Stars na hure kwa viongozi kwa makocha na benchi la ufundi.
Umahiri mkubwa wa wachezaji wetu, ukuta imara wa safu ya ulinzi aaah! Kwa hakika vilisaidia katika ushindi huu.
Stars itaungana na nchi nyigine 17 kutoka mataifa anuwai ya Afrika huko nchini Ivory Coast zitakapopigwa Fainali hizo.
Hii imetajwa kuwa ni mara ya 3 kwa Stars kutinga hatua hiyo.⚽👏👏👏
Rais Dkt.Samia kutoa Shumbe ya Milioni 500
Kama ilivyo kawaida yake. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, amekuwa na mchango mkubwa sana katika kuinuia soka na michezo ya Tanzania 🇹🇿 kwa ujumla wake.
Amekuwa akitoa motisha kwa vilabu mbalimbali, timu mbalimbali za Taifa na timu kuu ya Taifa.
Katika kuunga mkono kwa Taifa Stars 🌟 kufuzu hatua hii ya kucheza fainali za AFCON aliwaahidi kutoa shumbe (kongole) ya Fedha za Kitanzania Shilingi Millioni 500 kwa timu hii Taifa Stars.
Heko Rais Dkt.Samia Suluhu kwa kuwatia shime vijana wa Stars kwa juhudi zao kubwa katika kufuzu kwenye michuano hiyo ya ngazi ya juu kwa Bara la Afrika.
Akitoa salamu hizo za shumbe hiyo Katibu mkuu wa wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Saidi Yakubu. Alisema tayari fedha hizo zimekwishapelekwa Wizarani. Baada ya kauli hiyo, ziliskika nderemo na vifijo kutoka kwa wachezaji wa Stars 🌟 na wadau wa soka wakisema mama, mama, mama, mama👏👏🙏
Heko Stars, heko TFF, heko wachezaji na kila mmoja aliyehusika na ushindi huu.👏👏👏 Kwa hakika mnastahiki maua yenu💐💐🌺🌷
Ushauri wetu wa jumla
- Kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano kwa viongozi wachezaji na wadau wote.
-Kuendelea kujiimarisha kiufundi na kushughulikia changamoto zote za kiufundi. Mathalan, safu ya ushambuliaji na kiungo ili kuongeza uimara wa kikosi.
-Kupata mechi nyingi za kirafiki ili kujiimarisha zaidi.
-Kuhakikisha tunachukua kombe hilo Yalayala tunafika hatua ya robo.💪💪🇹🇿
-Kuunda kamati za hamasa, vikundi ili kuipa hamasa timu.
-Kuendelea kuimarisha uhusiano mwema zaidi na serikali, wadhamini, wanahabari, wadau wote muhimu ili kuzidi kupata fursa zitokanazo na wao na kuiboresha kikosi.n.k
Kongoleni sana Stars, Kongoleni Shirikisho la soka la Tanzania TFF, Kongole Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa motisha Kongoleni sana Watanzania 👏👏☘️ kwa mafaniko haya.
Mafanikio haya ni kichocheo kikubwa katika kuitangaza zaidi nchi yetu kimataifa na kidunia.
Kwa hakika mmetuvesha nguo.