ZINAZOVUMA:

Mahakama yatoa uamuzi, yabariki uwekezaji bandari

Mahakama Kuu kanda ya Mbeya Leo imebariki mkataba wa IGA...

Share na:

Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya leo Alhamisi Agosti 10, 2023 imebariki mkataba wa IGA kuwa ni halali na imesema malalamiko yaliyowasilishwa hayana mashiko.

Uamuzi huo umetolewa katika kesi ya kupinga mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii Kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai (IGA).

Baada ya Mahakama kutoa uamuzi huo, walalamikaji katika kesi hiyo wamesema wanajipanga kukata rufaa kuupinga uamuzi huo.

Alphonce Lusako ambaye ni mlalamikaji wa kwanza katika kesi hiyo iliyotolewa uamuzi leo Alhamisi Agosti 10, 2023 amesema; “Tumesikia kigugumizi cha Mahakama, tumeshamwelekeza wakili wetu tutakata rufaa na tutawasilisha leo hii notisi ya kukata rufaa,” amesema.

Wakili aliyesimamia upande wa walalamikaji katika kesi hiyo, Boniphace Mwabukusi amesema wanatoa siku 14 Serikali kubadili mkataba huo.

“Kwa kuwa Mahakama imesema haina mamlaka ya kuingilia shughuli za Bunge sasa sisi tunakwenda kutumia Civil Bunge (Bunge la Wananchi) tutatoa siku 14 wabadiki mkataba huu,” amesema.

Mwabukusi ameongeza kuwa wanajipanga kwenda Mahakama ya Rufani.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya