Baada ya mvutano wa muda mrefu hatimae Mahakama ya Juu nchini Mexico imehalalisha utoaji wa mimba kote nchini humo.
Hatua hiyo inajiri baada ya miaka miwili ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wa kuunga mkono pingamizi la sheria iliyopo katika jimbo la kaskazini la Coahuila.
Mahakama hiyo ilitoa uamuzi kuwa adhabu za uhalifu kwa utoaji wa mimba zilikuwa kinyume na katiba.
Majimbo ya Mexico na serikali kuu tangu wakati huo yamekuwa na sintofahamu juu ya kufuta kanuni za adhabu.
Uamuzi huo mpya wa hivi sasa unahalalisha utoaji mimba katika majimbo yote 32 ya Mexico.
Mahakama ya Juu Zaidi ilisema kukataliwa kwa uwezekano wa kutoa mimba kulikiuka haki za binadamu za wanawake.
“Katika kesi za ubakaji, hakuna msichana anayeweza kulazimishwa kuwa mama sio na serikali wala na wazazi wake au walezi wake,” mkuu wa mahakama hiyo, Arturo Zaldívar alisema.