ZINAZOVUMA:

Mahakama yaamuru Tanzania kufuta adhabu ya viboko

Mahakama ya haki za Binadamu Afrika yaamuru Tanzania kufuta adhabu...

Share na:

Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu yaiamuru Tanzania, kuondoa adhabu ya viboko katika sheria zake.

Katika kuanzisha Mahakama hiyo Tanzania na nchi nyingine zilizokubali mahakama hiyo, zilisaini mkataba uliopinga adhabu ya viboko.

Hata hiyo bado Tanzania, imekuwa ikitoa adhabu adhabu ya viboko kwa wafungwa.

Hivyo jopo la majaji 11 liliamuru Tanzania, kuwasilisha ripoti kila baada ya miezi 6 juu ya hali ya utoaji wa adhabu mbalimbali nchini.

Majaji hao wamendelea na kusemakuwa juu ya ukomo wa ripoti hizo ni, “hadi pale taasisi hiyo itakapozingatia kuwa kumekuwa na utekelezaji kamili”.

Mkataba huo haukubagua baadhi ya adhabu za viboko, bali ilichukulia adhabu zote za viboko kwa wafungwa na hata katika maisha ya kawaida kama shule na kwingineko.

Hatua hii ya mahakama inatokana na kanuni za Tanzania, kuorodhesha viboko kama ni moja ya adhabu katika baadhi ya makosa.

Miongoni mwa makosa yenye adhabu ya viboko ni ubakaji, na wizi wa silaha kama ilivyowahi kutolewa kwa baadhi ya wafungwa.

Pia mahakama hiyo iliamuru kulipwa fidia mmoja wa waathirika wa adhabu hiyo ya viboko.

Imeamuriwa Yassin Rashid Maige kulipwa dola za marekani 119, sawa na Shilingi laki tatu za Tanzania kama fidia yy unyanyasaji wa kimaadili.

Viwango vya kubadili fedha $1= 2500TZS

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya