Mahakama Kuu ya Islamabad nchini Pakistan imebatilisha hukumu waliyopewa Imran Khan na Shah Mahmood Qureshi katika maarufu ya Cypher.
Inaaminika kuwa sakata hilo linalowahusisha wawili hao liltokea wakati Imran Khan ni Waziri Mkuu na Shah Mahmood Qureshi akiwa ni Waziri wa Mambo ya Nje.
Wawili hao walikata rufaa Mahakama Kuu baada ya mahakama maalum ya Rawalpindi, kuwahukumu kifungo cha miaka 10 gerezani mwezi Januari mwaka huu.
Jaji Mkuu Aamer Farooq na Jaji Miangul Hassan Aurangzeb wa mahakama Kuu, wamekubali rufaa yao iliyowafurahisha wengi hasa wafuasi wa Chama cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI).
Hata hivyo bado Imran Khan anaweza kubaki gerezani kutokana, kutokana na kesi waliyofunguliwa yeye na Mkewe Bushra Bibi kuwa ndoa yao ya mwaka 2018 inakiuka sheria za Kiislam.
Pamoja na Qureshi kuwa hana kosa kwa sasa haijulikani kama ataruhusiwa kutoka gerezani au hatoruhusiwa.