ZINAZOVUMA:

TMA yatangaza uwepo wa El Nino

El Nino inaweza kupiga kuanzia Oktoba amesema Dk. Kantamla Meneja...

Share na:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema, El Nino inatarajiwa kuwepo katika kipindi cha mvua za vuli zitakazoanza kunyesha Oktoba hadi Desemba. Inatazamiwa mvua wa vuli kwa mwaka huu zitasababisha athari kubwa katika maeneo mbalimbali nchini kutokana na kuambatana na El Nino.

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatano Julai 19, 2023 na Meneja mkuu wa Utabiri, Dk. Mafuru Kantamla. Dk. Kantamla ameendelea kusema kuwa hadi kufikia sasa inaonyesha imefikia asilimia 90 ya kuwepo kwa mvua hizo kubwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Dk. Kantamla aliyataja maeneo ambayo yataathirika na mvua hizo ni mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara.

“Ongezeko la mvua linasababisha kutabiri uwepo wa El Nino, mfano kipindi cha kipupwe tumeona imeanza kujitengeneza athari zake hatutegemei kipindi hiki ongezeko la mvua kubwa,” amesema Dk. Kantamla.

Pia, Dk Kantamla amesema, haitaathiri wakazi wa bahari ya hindi pekee, bali itasambaa hadi maeneo ya nyanda za juu Kaskazini na ukanda wa Pwani.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya