Kushindwa kwa Serikali kutoa huduma za msingi kwa wananchi kumechochea kuibuka kwa migogoro katika baadhi ya nchi za Afrika, ikiwa ni pamoja na kupelekea kuundwa kwa mifumo ambayo inadhoofisha mamlaka za Serikali kwa kuanzisha mifumo ambayo inaeneza matakwa ya wananchi kwa njia ya vurugu.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo katika ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Demokrasia Afrika mkoani Arusha akisema mifumo hiyo ni kama wanaharakati, makundi ya kigaidi, maandamano, ambayo inapelekea uhuru wa kukusanyika na kujieleza kutumika vibaya.
Ameongeza kuwa hadi hapo nchi za Afrika zitakapoweza kutatua changamoto za utawala wa kidemokrasia na kufikisha huduma za msingi kwa wananchi, demokrasia itabaki kuwa tamanio ambalo halitofikiwa katika ukamilifu wake.