Kampuni ya nafaka ya Cargill yenye makao yake nchini Marekani, imetangaza kuuza hisa zake katika Temino ya nafaka nchini Urusi.
Mnunuzi wa hisa hizo ni kampuni ya Delo Group, ambayo inajihusisha na usafirishaji nchini Urusi.
Kampuni hiyo imeamua kuuza hisa zake katika kampuni ya KSK, inayoendesha temino ya mazao jijini Novorossiysk.
Kampuni ya Cargill ilikuwa na umiliki wa asilimia 25 katika kampuni ya KSK nchini Urusi.
Hata hivyo msemaji wa Cargill hakutoa taarifa yoyote juu ya kiasi cha fedha kilichotumika katika mauziano hayo.
Hata hivyo kutokana na maelezo yake inaonyesha kuna makubaliano ya ndani kwa kampuni ya Cargill kusitisha biashara yake nchini Urusi.
Huku ikitazamiwa kuwa huenda kuna msukumo Zaidi kutoka katika mamlaka za biashara nchini marekani.
Hali inayosababisha kampuni nyingi kuuza au kusitisha opereshi zake nchini Urusi, kutokana na Urusi kuvamia Ukraine.
Muwakilishi wa kampuni ya Delo alisema kuwa kamisheni ya uwekezaji wa nje ya Urusi inafanyia kazi mauziano hayo.
Na kuongeza kuwa wanategemea mchakato huo kukamilika baada ya mwezi mmoja.
Hii itakuwa ni kampuni ya pili kuuza hisa zake kwa Delo Group, mwezi februari mwaka huu kampuni ya Maersk iliuza hisa zake za kampuni ya Global Ports Investments kwa Delo Group.