ZINAZOVUMA:

Ukraine na Rwanda kushirikiana

Ukraine na Rwanda wametia saini mkataba wa kushirikiana katika biashara,...

Share na:

Rwanda na Ukraine zimetia saini mkataba wa maelewano kuhusu mashauriano ya kisiasa na kujadili maeneo mengine ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Mkataba huo ulitiwa saini na waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Vincent Biruta, na mwenzake wa Ukraine Dmytro Kuleba, baada ya wawili hao kufanya mkutano.

Kuleba alikuwa nchini Rwanda kwa ziara ya siku ambapo moja katika ziara yake ya pili barani Afrika ambayo pia imemkuta akitembelea Morocco na Ethiopia.

“Tunakusudia kuongeza ushirikiano katika biashara, uwekaji digitali, anga, ujenzi, elimu, na dawa.

Ukraine itafungua ubalozi nchini Rwanda,” Kuleba alinukuliwa akisema.

Kulingana na wizara ya mambo ya nje ya Ukrane, Kuleba na Biruta pia walijadili hali ya amani ya Ukraine, usalama wa chakula barani Afrika, mauzo ya nafaka ya Ukraine kupitia Bahari Nyeusi na mpango wa kibinadamu wa Nafaka Kutoka Ukraine.

Kuleba baadaye alikutana na Raisi wa Rwanda Paul Kagame na akaweka wazi nia kubwa ya Ukraine katika kuendeleza uhusiano na Rwanda.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya