Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un anapanga kusafiri hadi Urusi mwezi huu kukutana na Rais Vladimir Putin kwa ajili ya mazungumzo yanayohusu silaha.
Viongozi hao wawili watajadili uwezekano wa Korea Kaskazini kuipatia Urusi silaha za kusaidia vita vyake nchini Ukraine, taarifa kutoka Marekani imesema.
Mahali halisi patakapofanyika mkutano uliopangwa haijulikani na hakukuwa na maoni yaliyotolewa kuhusu ripoti hiyo, ambayo pia iliangaziwa na vyombo vingine vya habari vya Marekani kutoka Korea Kaskazini na Urusi.
Vyanzo vya habari vililiambia gazeti la New York Times kwamba Rais Kim ana uwezekano mkubwa wa kusafiri kwa treni ya kivita mpaka Urusi.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika unawadia baada ya Ikulu ya White House kusema kuwa ina habari juu ya mazungumzo ya silaha kati ya nchi hizo mbili.
Aidha taarifa zinasema kuwa Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu aliishawishi Korea Kaskazini kuiuzia Urusi risasi za kivita wakati wa ziara yake aliyoifanya hivi karibuni nchini nchini humo.