ZINAZOVUMA:

Marufuku kutumia ‘WhatsApp’ kutuma nyaraka za serikali

Matumizi ya WhatsApp yamepigwa marufuku kutumika katika kutuma nyaraka za...

Share na:

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete amesema sheria inayosimamia nyaraka za Serikali inaelekeza kuwa mawasiliano ya Serikali yafanyike kwa njia ya barua na si vinginevyo.

Kufuatia kuwepo kwa sheria hiyo, Naibu Waziri Kikwete amewaonya watendaji wa Serikali ambao wanatumia njia ambazo sio rasmi kutuma nyaraka.

“Haitokuwa sawa na ni marufuku ya Serikali kuwasilisha au kutumiiana ‘Documents’ za Serikali kupitia njia ya WhatsApps na njia nyingine zisizo rasmi, isipokuwa kwa maelekezo ambayo yatakuwa yametolewa vinginevyo katika mamlaka,” amesema Naibu Waziri Ridhiwani Kikwete.

Ameyasema hayo Bungeji jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Janejelly Ntate James ambaye amehoji uhalali wa matumizi ya makundi ya WhatsApp kutumiana nyaraka.

Aidha, Naibu Waziri Kikwete amelihakikishia Bunge kuwa Serikali bado inaendelea kutengeneza mifumo mbalimbali ambayo itaileta Serikali yote katika adabu ya utendaji.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya