ZINAZOVUMA:

Hakuna kiingilio, Stars vs Uganda.

TFF imetangaza kuwa hakutakuwa na kiingilio katika mechi ya Taifa...

Share na:

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetangaza milango kuwa wazi katika mechi ya kesho ya Taifa stars dhidi ya Uganda kwa upande wa mzunguko Kwa kuwa tayari tiketi zote za mzunguko zimeshalipiwa.

Afisa habari wa TFF, Clifford Ndimbo amesema kufika kwako mapema itakua ndio tiketi yako na milango itakua wazi kuanzia saa sita mchana.

Ndimbo amesema kama tiketi zingekua chache basi wangetangaza utaratibu wa namna ya kuzipata lakini kwakua zimeshalipiwa basi nafasi ipo wazi kwa kila mtanzania kuingia uwanjani.

Aidha ameishuruku serikali na wadau walionunua tiketi hizo huku akiwahimiza mashabiki kuhakikisha wanajaa uwanjani kwa wingi.

Mchezo utakaochezwa kesho utakua ni wa marudiano baada ya mchezo wa kwanza Taifa stars kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila dhidi ya Uganda uliopigwa nchini Misri.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya