ZINAZOVUMA:

kisa mapinduzi Gabon yaondolewa Jumuiya ya Madola

Jumuiya ya Madola imeiondoa nchi ya Gabon kwa muda kutokana...

Share na:

Nchi ya Gabon imeondolewa kwa muda katika Jumuiya ya Madola baada ya viongozi wa kijeshi kufanya mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Rais Ali Bongo.

Uamuzi huo umetolewa na mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya Madola waliokutana pembezoni mwa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa unaoendelea jijini New York, Marekani.

Viongozi hao wametoa wito kwa nchi ya Gabon kuzingatia maadili na kanuni za Jumuiya ya Madola.

Aidha Wameiomba nchi hiyo kufanya uchaguzi wa demokrasia na wa kuaminika haraka iwezekanavyo ili waweze kurudishwa kwenye Jumuiya.

Jeshi la Gabon lilimwondoa Raisi Bongo madarakani muda mfupi tu baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa 2023.

Raisi Bongo amekuwa akiongoza nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta tangu mwaka 2009, alipomrithi babake ambaye alietawala kwa miaka 41.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya