ZINAZOVUMA:

Kagame: Urusi ina haki ya kuwa popote barani Afrika.

Raisi wa Rwanda Paul Kagame amesema nchi ya Urusi ina...

Share na:

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema Urusi ina haki ya kuwa popote barani Afrika, kama tu ilivyo kwa nchi nyingine yoyote ile.

Akiwa ziarani katika mataifa ya Afrika Magharibi, Rais Kagame amezungumzia wazi vita vinavyoendelea nchini Ukraine kwa kusema nchi za Magharibi zinajaribu kuiburuza Afrika katika matatizo yake, kwani baadhi ya nchi za Kiafrika zimechagua kutoegemea upande wowote katika suala hilo.

Amesema nchi za Magharibi zimekuwa zikilalamika kuhusu uwepo wa China na Urusi barani Afrika, na bara hilo linapaswa kutambua mahitaji yake katika suala la ushirikiano wa kimataifa na kuwageukia wale wanaotoa kile wanachokihitaji.

Kwa mujibu wa rais huyo wa Rwanda, Afrika inajaribu kutatua matatizo yake yenyewe ambayo yanaigusa moja kwa moja, yasiyo na uhusiano wowote na nchi moja kubwa.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya