ZINAZOVUMA:

JUDITH SUMINWA Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke DRC

Bi. Judith Suminwa Tuluka aliyekuwa Waziri wa Mipango nchini DRC...

Share na:

Waziri wa mipango wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Judith Suminwa Tuluka Jumatatu amekuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke katika taifa hilo la Afrika ya kati, televisheni ya serikali imetangaza.

Waziri huyo mkuu mpya, ni mchumi na amechukuwa nafasi ya Jean Michel Lukonde kufuatia ushindi wa kishindo wa muhula wa pili wa Rais Felix Tshisekedi kwenye uchaguzi wa tarehe 20 Disemba mwaka jana.

Tuluka alisema kupitia televisheni ya taifa kwamba “kazi ni kubwa, changamoto ni kubwa lakini kwa pamoja tutafika”.

“ Ninafahamu jukumu kubwa linalonisubiri,” aliongeza, akisema anataka kufanya kazi “kwa ajili ya amani na maendeleo” ili “wananchi wa Congo wanufaike na rasilimali” za nchi.

Tshisekedi alishinda rasmi kwa asilimia 73.47 kwenye uchaguzi wa Disemba ambao ulifanyika kwa amani kwa kiasi kikubwa katika nchi inayokumbwa na ghasia na ukosefu wa usalama, uchaguzi ambao upinzani ulidai uchaguzi uligubikwa na udanganyifu.

Waziri mkuu mpya atakuwa na jukumu la kutekeleza vipaumbele vilivyotangazwa na rais kuhusu ajira, vijana, wanawake na uwiano wa kitaifa katika taifa hilo la takriban watu milioni 100.

Tshisekedi alikuwa rais mwaka 2019 akiahidi kuboresha maisha nchini DRC, nchi yenye utajiri wa madini lakini yenye raia wengi maskini, na kumaliza umwagaji damu wa miaka 25 mashariki mwa nchi.

Pia kwa kuwa haijasemwa ni nani atashika nafasi ya Waziri wa mipango, haijafahamika kama mama huyo atahudumia nafasi hizo zote mbili kwa wakati mmoja kama ambavyo imeonekana mifano ya Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Dotto Biteko akishika pia nafasi ya Waziri wa Nishati au atachaguliwa mtu mwingine kushika wizara ya Mipango nchini DRC.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya