ZINAZOVUMA:

JKT inatoa fursa ya ajira kwa vijana

Rais Samia Suluhu Hassan amelipongeza Jeshi la kujenga Taifa kwa...

Share na:

Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa JKT inatengeneza ajira ili kuwawezesha Vijana kupunguza kiwango cha umasikini na utegemezi nchini.

Amesema hayo wakati aliposhiriki Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Leo Julai 10, 2023 ambapo Viongozi mbalimbali walihudhuria huku tuzo za heshima zikitolewa.

“Nafarijika kuona sasa kuna mwitikio mzuri wa Vijana kujiunga na Jeshi hili, JKT imefanya kazi kubwa na za kuonekana, wamejenga ukuta wa kulinda madini ya Tanzanite Mererani, wamejenga Mji wa Serikali Mtumba, ujenzi wa Ikulu ya Chamwino na miradi mingine, tunawapongeza sana JKT”

“JKT inawafungua Vijana kuingia maeneo mengine ya kazi na kuweza kujitegemea, Jeshi hili linatengeneza ajira ili kuwawezesha Vijana kupunguza kiwango cha umasikini na utegemezi, Nchi yetu iwe inaweza kujiendesha yenyewe”

Aidha Rais Samia ametoa maelekezo kwa Wizara ya Ulinzi kuandaa mpango mkakati wa kurekebisha kambi za vijana wa JKT huku ikianza na upande wa maelezi ya Vijana, pia kuwezesha Suma JKT kama Shirika kupata mikopo ili kuweza kujiendesha.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya