ZINAZOVUMA:

IRAN: Marekani anachochea vita Ukraine na imejaribu kunipindua

Raisi wa Iran ashutumu Marekani kwa uchochezi kwenye vita vya...
Raisi Wa Iran Ebrahim Raisi akionyesha picha ya Jenerali wa Iran anayesadikiwa kuuliwa na Marekani katika hotuba yake ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika makao Makuu ya UN Jijini New York Sept. 21, 2022. (AP Photo/Mary Altaffer)

Share na:

Rais wa Iran Ebrahim Raisi ameishutumu Marekani kuchochea vita vya Ukraine na Urusi.

Ameyasema hayo katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) alipokuwa akihutubia.

Raisi alidai ndege zisizo na rubani zinazoipiga miji ya Ukraine, ziliuzwa kabla ya vita kuanza na kusema kuwa wanaiombea amani Ukraine.

Miongoni mwa sababu alizosema za Marekani kuchochea vita vya Ukraine, ni mpango wa marekani kudhoofisha ulaya.

Katika hotuba yake pia, ameishutumi Marekani kufanya jitihada mbalimbali za kuangusha utawala wake.

Na kusema kuwa amepishana na viunzi vingi, vilivyowekwa na marekani dhidi ya utawala wake.

Wakati raisi akiendelea na hotuba yake, muwakilishi wa Israel bw. Gilad Erdan alisusa na kutoka nje ya ukumbi.

Marekani nayo ilijibu mapigo ya hituba hiyo, kwa kuendelea kuongeza vikwazo vipya kwa watu binafsi na mashirika kutoka Iran, China, Urusi na hata Uturuki.

Hii ni baada ya majeshi ya Urusi kushambulia kwa ndege kubwa zisizo na rubani kwenye miji ya Ukraine.

Vikwazo hivyo vililenga watu na mashirika yaliyohusishwa na kuunda ndege hizo kubwa zisizo na rubani.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Siasa nchini Iran bw. Bagheri Kani amekutana na wawakilishi kutoka Ujerumani, Ufaransa na Uingereza (E3).

Huku ajenda kuu ya mkutano huo wa bagheri, ukilenga kutaka kuizuia Iran isitekeleze mpango wake, wa kufukuza theluthi ya wachunguzi wa silaha toka UN.

Wakisema kuwa wakifukuzwa wachunguzi hao wa Umoja wa Mataifa, itashindikana kuchunguza na kudhibiti matumizi ya silaha kwa raia nchini humo.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,