ZINAZOVUMA:

Hunter Biden na kesi ya jinai katikati ya kampeni za Baba yake

Hunter Biden mtoto wa pili wa Rais Biden ameshitakiwa kwa...

Share na:

Mtoto wa Biden ajulikanaye kwa jina la Hunter Biden amekumbwa na kesi ya uhalifu wa silaha, katika kipindi ambacho baba yake yupo kwenye kampeni za Urais nchini humo.

Kesi hiyo inayotarajiwa kusikilizwa siku ya Jumatatu, inaweza uathiri mwenendo mzima mchakato wa Biden kurudi Ikulu.

Hii ni kwa mara ya kwanza kwa mtoto wa Rais wa Marekani anayehudumu kushitakiwa katika historia ya taifa hilo.

Wakili David Weiss, aliteuliwa mwaka jana kama wakili maalum wa kusimamia uchunguzi wa Hunter mwaka jana, aliwasilisha mashtaka kwa niaba ya Idara ya Sheria.

Hunter Biden mwenye miaka 54, anashutumiwa kukiuka sheria ya shirikisho kwa kununua na kumiliki bunduki wakati akiwa na kwenye matumizi ya dawa za kulevya.

Ingawa amekuwa wazi kuhusu vita vyake na uraibu wa pombe na madawa ya kulevya, alikana hatia ya makosa hayo matatu.

Kwa makosa yake Hunter anaweza kukaa jela miaka 25, iwapo atapatikana na hatia katika makosa yote matatu.

Ingawa mbali na makosa hayo anayokabiliwa nayo, hakuna rekodi nyingine za uhalifu za nyuma alizokutwa nazo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya