ZINAZOVUMA:

Benjamin Mendy hana hatia tuhuma za ubakaji

Mchezaji wa zamani wa Manchester City Benjamin Mendy amekutwa hana...

Share na:

Mchezaji wa zamani wa Manchester City Benjamin Mendy amekutwa hana hatia katika mashtaka ya kumbaka mwanamke na jaribio la kumbaka mwanamke mwingine.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alishtakiwa kwa kumbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 24 katika jumba lake la kifahari lilipo mjini Mottram St Andrew, Cheshire mnamo Oktoba 2020.

Mendy pia alishtakiwa kwa jaribio la kumbaka mwanamke mwingine, mwenye umri wa miaka 29, ambaye pia alisema kuwa alimdhalilisha nyumbani kwake miaka miwili iliyopita.

Wakati wa hukumu hiyo inatoka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliangua kilio baada ya kesi hiyo kudumu kwa wiki tatu katika Mahakama ya Chester Crown.

Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City alihusisha na makosa mengi ya ubakaji ambayo yote amekutwa hana hatia.

Kwa upande mwingine wengi wanadhani kinachoendelea dhidi ya Benjamin ni kutokana na rangi yake na abambikizwa kesi sababu yeye ni mweusi.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya