ZINAZOVUMA:

Helping Hand yaleta furaha kwa wanafunzi

Taasisi ya 'Helping Hand for relief and Development Africa' imegawa...

Share na:

Taasisi ya ‘Helping Hand for Relief and Development Africa’ inayojihusisha na masuala ya kijamii na Maendeleo imefanikiwa kugawa viti na meza kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya sekondari ya Mpapa iliyopo Zanzibar.

HHRD‘ imeweka wazi kuwa Shule nyingi za sekondari zinakabiliwa na changamoto ya madawati na miundombinu mizuri hali inayoathiri maendeleo yao kwa kiasi kikubwa.

‘Helping Hand’ ilifanikiwa kugawa samani hizo ambazo zitatumika na wanafunzi hao katika kujifunzia ili kukuza na kuboresha namna ya upatikanaji wa elimu shuleni hapo.

Kwa upande wake uongozi wa shule umetoa shukrani zake kwa taasisi hiyo kwa mchango huo na wameupokea kwa mikono miwili kwani utaboresha matokeo ya vijana wao.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya