Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Jokate Mwegelo amekabidhi baiskeli 200 kwa wanafunzi wa kike wa shule 10 za sekondari zilizopo katika Halmashauri ya Korogwe vijijini ambao wanakabaliwa na changamoto ya kutembea umbali mrefu wa zaidi ya Km 20 hadi Shuleni hali ambayo inapelekea Baadhi yao kukatisha masomo kutokana na Ujauzito
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi baiskeli zilizotolewa na Shirika la Uratibu na Ushirikiano la Uturuki (TIKA) Mkuu wa Wilaya hiyo Jokate Mwegelo amesema Zitawasaidia watoto wa kike kufika shuleni kwa wakati na Kuondokana na utoro wa mara kwa mara kutokana na umbali mrefu wanaotembea hadi kufika shuleni.
DC Jokate amesema wanamshukuru Balozi wa Uturuki hapa nchini Dr Mehment Gulluoglu kwa kuunga mkono juhudi za Mh Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuboresha mazingira ya elimu kwa watoto wa kike kwani imetoa hamasa kwa watoto hao kusoma kwa bidii.