ZINAZOVUMA:

Hatimaye Mtoto wa Museveni awa Mkuu wa Majeshi

Mtoto wa Ris Museveni, Muhoozi Kainerugaba maarufu kwa machapisho ya...

Share na:

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amemteua mtoto wake, Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Gazeti la Daily Monitor la Uganda limeripoti.

Anachukua nafasi ya Jenerali Wilson Mbasu Mbadi ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa biashara katika mabadiliko mapya ya safu ya Baraza la mawaziri lililotangazwa karibuni.

Jenerali Muhoozi alikuwa akihudumu nafasi ya mshauri mkuu wa Rais katika masuala ya operesheni maalumu.

Jenerali Muhoozi amekuwa maarufu kwa kuchapisha vitu mbalimbali vinavyotamiwa kuwa ni nje ya matagemeo ya watu kwake kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii hasa mtandao wa X zamani Twitter.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,