ZINAZOVUMA:

Hali ya dharura kwa mwaka mmoja yatangazwa Libya

Hali ya hatari imetangaza nchini Libya juu ya maambukizi mapya...
Rescue teams search for victims in Derna, Libya, on Sunday, Sept. 17, 2023. Libyan authorities have opened an investigation into the collapse of two dams that caused a devastating flood in a Derna as rescue teams searched for bodies on Saturday, nearly a week after the deluge killed more than 11,000 people. (AP Photo/Yousef Murad)

Share na:

Serikali nchini Libya imetangaza hali ya dharura ya mwaka mzima kwa lengo la kuzuia kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko.

Wiki iliyopita, kimbunga cha “Daniel” kilipiga maeneo kadhaa ya miji ya Benghazi, Al-Bayda, Marj, Susa, Shahatt na Derna.

Shirika la Afya Duniani limeonya kuhusu kuenea magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokumbwa na kimbunga na mafuriko hayo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, Mkuu wa Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Magonjwa nchini Libya, Haidar al-Sayeh alitoa taarifa na kutangaza idadi ya sumu ambazo zimeripotiwa kutokana na matumizi ya maji ya kunywa huko Derna.

Akizungumzia kutotumika maji ya kunywa katika jiji la Derna, Al-Sayeh amesema kuwa, hali ya hatari ya mwaka mmoja itatangazwa katika maeneo yaliyoathiriwa na dhoruba na mafuriko.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya