Mitaa ya jiji la Dar imekuwa giza totoro usiku wa leo(22 Agosti 2023), kutokana na hitilafu katika mitambo ya kuzalisha umeme ya Ubungo II.
Kutokana na hitilafu hiyo, Tanesco makao mkuu (Dodoma), imetoa taarifa kwa umma juu ya katizo hilo la umeme.
Maeneo yaliyoathirika ni mikoa ya Dar es Salaam na mikoa yote ya Zanzibar.
Hitilafu hiyo imesababisha kukosekana zaidi ya megawatt 260 katika gridi ya taifa, hali iliyosababisha Dar na baadhi ya mikoa kuwa nia giza totoro nyakati za leo usiku.
Kulingana na taarifa ya TANESCO ya saa 3 asubuhi, walitegemea kutatua hitilafu hiyo ndani ya masaa manne.
Hata hivyo hawakufanikiwa kutatua changamoto hiyo na kulazimika kutoa taarifa nyingine saa 9 alasiri.
Katika taarifa ya pili, Mkurugenzi wa huduma kwa wateja bw. Martin Mwambene amesema kuwa “… mafundi wao wanajitahidi kushughulikia tatizo hilo. Na wanatarajia kulitatua kabla ya siku kuisha.”