Wabunge nchini Ghana wamepitisha Muswada wa Sheria itakayoruhusu Kilimo cha Bangi kwa matumizi ya Dawa, Viwandani na Biashara nje ya nchi hiyo.
Kwa Sheria hiyo mpya sasa, Serikali ya Ghana itaachana na mazoea na kuungana na Mataifa mengine takriban 10 ya Afrika yaliyoamua kuhalalisha Bangi kwa matumizi ya Dawa, Viwandani na Biashara nje ya Nchi.
Pamoja na ruhusa hiyo, mimea ya Bangi itakayozalishwa chini ya sheria hiyo itakuwa na kiwango maalum cha Kichangamshi kinachosababisha mtumiaji au mvutaji kujisikia Kulewa au kupata hisia tofauti na hali ya kawaida.
Ndani ya miaka 5 Nchi za Lesotho, Zimbabwe, Afrika Kusini, Uganda, Malawi, Zambia, Ghana, eSwatini, Rwanda na Morocco zimeruhusu Kilimo cha zao hilo ambalo linatajwa kuwa Viambata vinavyotibu Saratani na Magonjwa mengine hatarishi.