ZINAZOVUMA:

G20 wagomea pendekezo juu ya tabia nchi

Baadhi ya wanachama wa G20 wagomea muswada wa Nishati na...
Moja ya Nembo za G20

Share na:

Mataifa wanachama wa G20 yaliyokuwa na mkutano wake nchini India mwaka huu, yameshindwa kuafikiana juu ya kupunguza kutumia nishati zenye kuharibu mazingira na tabia nchi.

Hii ni baada ya baadhi ya nchi wanachama wanaozalisha nishati hizo kupinga azimio hilo.

Mkutano huo uliazimia wanachama wake kuchanga dola Bilioni mia ($100B) kila mwaka kuanzia mwaka 2020 hadi 2025.

Fedha hizo zipelekwe katika mataifa yanayoendelea ili kupambana dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Wanasayansi na wanaharakati wengi wa mazingira wamesikitishwa baada ya kuona wakubwa hao wa dunia wakigoma kupunguza uzalishaji na matumizi ya nishati hizo.

Baada ya mkutano huo mambo 22 katik ya 29 yaliyotegemewa kujadiliwa yaliafikiwa na wanachama wote, huku saba yakibaki katika “Chair Summary”.

Katika muhtasari wa mwenyekiti uliotoka jumamosi jioni umesema kuwa “wengine wana maoni tofauti juu ya kuunguza na teknolojia za kuondoa (hewa ukaa) zinaweza kufikia panapohitajika”.

Hata hivyo mataifa yanayoshukiwa kukataa azimio la nishati na tabia nchi ni pamoja na Saudi Arabia, Afrika Kusini, Indonesia, China pamoja na Urusi.

nchi hizi zimeshukiwa kutokana na uzalishaji wake au matumizi, ingawa muhtasari huo haukuweka wazi mataifa gani yalipinga muswada huo.

Pia katika mkutano huo mataifa hayo, yalikosa makubaliano ya pamoja juu ya Vita vya Ukraine.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya