ZINAZOVUMA:

Mabadiliko ya tabia ya nchi kuhatarisha ukuaji wa kilimo

Waziri wa kilimo Mhe Hussein Bashe amesema mabadiliko ya tabia...

Share na:

Waziri wa Kilimo, Mhe Hussein Bashe amesema kihatarishi namba moja kwa taifa hivi sasa itakuwa ni mabadiliko ya tabianchi ambayo yanasababisha kupungua kwa uzalishaji wa chakula na hivyo kuhatarisha uimara wa uchumi wetu na usalama wa Taifa letu.

Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2023/24, amesema:

“Ili kuwa salama kwenye eneo hili ni lazima kuendelea kuwekeza katika mifumo imara na himilivu ya kilimo inayotumia teknolojia za umwagiliaji za kisasa,uwezo wa kuhifadhi mbegu zetu za asili ili kuwa msingi imara wa kufanya utafiti kupata teknolojia bora za uzalishaji wa mbegu ili kujihakikishia usalama wa chakula na ulinzi wa uchumi wetu”.

Aidha Waziri Bashe amesema Serikali imewawezesha vijana 250 kwenda nchini Israel kwa ajili ya kupata mafunzo ya kilimo kwa vitendo katika mashamba makubwa ili waweze kujiajiri na kutoa huduma na ushauri kwa wakulima watakapohitimu.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya