ZINAZOVUMA:

Demokrasia ya Magharibi haifanyi kazi Afrika

Kiongozi wa kijeshi kutoka Guinea amesema nchi za Magharibi ziache...

Share na:

Kiongozi wa kijeshi wa Guinea, Kanali Mamady Doumbouya, amesema mtindo wa Magharibi wa demokrasia haufanyi kazi barani Afrika.

Ameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York kwamba bara hilo lilikuwa likiteseka kutokana na kuiga demokrasia yao ya Magharibi ambayo haiendani na uhalisia.

“Wakati umewadia muache kutuelekeza na kutufanya kama watoto,” aliongeza.

Kanali Doumbouya alichukua mamlaka katika mapinduzi ya kijeshi mwaka wa 2021, na kumuondoa madarakani Rais Alpha Condé.

Alitetea hatua hiyo ya mapinduzi ya kijeshi katika kikao cha Umoja wa Mataifa akisema ni kuokoa nchi zetu kutokana na machafuko kamili.

Wakati anaichukua nchi Kanali Doumbouya habari za mapinduzi zilipokelewa kwa furaha na umati wa watu katika mji mkuu, Conakry kwani wengi walikuwa wamefarijika kwamba Rais Condé alikuwa ameondolewa madarakani.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya