ZINAZOVUMA:

Baadhi ya maeneo kukosa umeme Dar kuanzia Septemba 1

Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limetangaza kuwa hakutakuwa na umeme...

Share na:

Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limetangaza kuwa kutakuwa na ukarabati na maboresho ya miundombinu kwenye njia kuu ya kusafirishia Umeme ya Msongo wa Kilovoti 132 Mbagala Dege na Kurasini.

Matengenezo hayo yatakua kuanzia siku ya Ijumaa, tarehe 01 Septemba 2023 na Jumapili,tarehe 03 Septemba, 2023 kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili za jioni.

Sababu ya kufanya ukarabati na maboresho hayo ni kuimarisha miundombinu ya umeme inayozunguka njia hiyo.

Kutokana na kazi hiyo TANESCO wamesema baadhi ya maeneo yatakosa huduma ya umeme kwa tarehe na muda tajwa kama ifuatavyo, baadhi ya maeneo ya Bandarini, Mbagala, Kurasini, Dege, Kibada, Mjimwema, Kisarawe II, Pemba mnazi, Avic town, Tuangoma na Geza ulole.

“Umuhimu wa kazi hii ni kuimarisha hali ya upatikanaji wa huduma ya umeme kwenye maeneo yanayopata umeme kutoka kwenye vituo vya kupoza Umeme vya Dege na Kurasini na hivyo kuwezesha ukuaji wa shughuli za kiuchumi” Imesema taarifa ya TANESCO.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya